Skip to main content

PROGRAMU HEDHI SALAMA -MANISPAA YA BUKOBA



HEDHI SALAMA
HALMASHAURI  YA  MANISPAA YA  BUKOBA

HEDHI SALAMA (Menstrual Hygiene Management )

Hedhi ni hali ya kawaida ya kimaumbile kwa motto wa kike ambayo ni ishara ya Afya bora. Ni kipindi cha kupevuka kwa mabinti kutoka katika hali ya utoto na kuingia hali ya ujana na baadae utu uzima.

MAFUNZO YALIYOMO
Ø  Hatua mbalimbali za makuzi kwa vijana wa kike na kiume (Kimwili, Kifikra na Kijamii) (mahusiano)
Ø  Mzunguko wa Hedhi unavyotokea (Menstrual wheel)
Ø  Kuvunja ukimya juu ya usimamizi wa Hedhi salama
Ø  Vifaa mbalimbali vya kujisitiri wakati wa Hedhi (Pedy na vitambaa safi vya kushona)
Ø  Vyombo vya kuhifadhia vifaa vya hedhi baada ya matumizi na namna ya kuvifukia/kuvichoma

KAURI MBIU JUU YA HEDHI SALAMA
Ø  Nitavunja ukimya juu ya Hedhi Salama, Sitaona aibu, nitajivunia na kutoa elimu hii ndani ya familia na kwa jamii nzima.
Ø  Zingatia usawa kijinsia kwa kuwashirikisha watu wenye mahitaji maalum (Walemavu wa viungo, viziwi, wasioona, walemavu wa akili na walemavu wa ngozi – Albino)

FAIDA ZA KUHIMIZA HEDHI SALAMA KWA MTOTO WA KIKE
Ø  Mtoto hujisikia huru awapo shuleni na nyumbani
Ø  Hupunguza utoro wa rejareja na wa kudumu (Uhudhuria siku 194 za masomo shuleni kwa mwaka mzima)
Ø  Hufanya vizuri kitaaluma
Ø  Humwepusha magonjwa mbalimbali
HASARA ZA KUTOKUWEPO KWA HEDHI SALAMA
Ø  Watoto wa kike kunyanyapaliwa wakiwa shuleni  kutokana na harufu mbaya
Ø  Kutohudhuria masomo na kurudi nyumba  kwa maendeleo  ya taaluma.
Ø  Kutojisikia huru  kwa  na wasiwasi wawapo hedhini
Ø  Kupatwa magonjwa mbalimbali mfano kuwashwa sehemu za siri

ZINGATIA:
Ø  HEDHI SALAM HAINA MBADALA
Ø  HEDHI SALAMA NI HAKI KWA KILA MTOTO WA KIKE NA MAENDELEO KIUCHUMI
Ø  PASIPO HEDHI HAKUNA MAISHA
Ø  HEDHI SALAMA NI NGUZO KWA KIZAZI CHA LEO NA KESHO
Ø  HEDHI NI ISHARA YA AFYA BORA
Ø  UPATIKANAJI WA MAJI SAFI  NI NGUZO KWA UTEKELEZAJI WA HEDHI SALAMA
Kumbuka: Siku ya hedhi husheherekewa duniani tarehe 28/05 kila mwaka
MHUSIKA MKUU WA SHUGHULI: MKURUGENZI WA MANISPAA YA  KUBOKA
MSIMAMIZI: Idara ya Elimu Msingi kwa kushirikiana na Idara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na watoto pamoja na Idara ya maji na Usafi wa Mazingira

MRATIBU: Mwezeshaji  Kitaifa wa Hedhi Salama-Afisa Elimu Sayansi Kimu na Afya wa Manispaa ya Bukoba na  mjumbe  wa Kamati ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba-Mwalimu Kibani.
WAELIMISHAJI: Wanafunzi wa vituo vya ufundi stadi (S/Kimu Nshambya), Sundi Elisha (S/Kimu Kibeta), Flavia Byashara-M/M S/M Ihungo, Inviolatha Rugashobora (Mchoraji mahiri S/M Rwemishasha “B”) na  Benedicto Gesusu Afisa Afya Halmashauri ya Manispaa ya  Bukoba na mjumbe wa Kamati ya Maji na Usafi wa Mazingira, Mwl Magreth Mukandara- mwakilishi wa watu wenye mahitaji maalum (S/M Buyekera) Pamoja na Afisa  Elimu  Kata Miembeni.

Comments

Popular posts from this blog